Posts

THT WAPATA PIGO R.I.P JESSY Q

Image
Aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva kutoka THT, Jessie, amefariki dunia. Jessie ni dada wa msanii, Jolie. www.eatv.tv imemtafuta mmoja kati ya wasanii kutoka THT, Mwasiti Almas ambaye amesema ni kweli kuwa msanii huyo amefariki dunia. Hata hivyo Mwasiti hakuelezea chanzo cha kifo chake kutokana na kutokuwa sehemu rafiki kwaajili ya mazungumzo na kuahidi kuwa ataeleza taarifa zaidi. "Ni kweli Jessie amefariki, lakini sipo sehemu nzuri kuzungumza kuna kelele sana", amesema Mwasiti. Marehemu Jessie enzi za uhai wake amewahi kufanya kazi kadhaa ikiwemo nyimbo ya 'Mapenzi Kamali' aliyomshirikisha Madee. Kwa mujibu wa taarifa za awali, kifo chake kimetokea hospitali wakati wa kujifungua

UKWELI KUHUSU KIFO CHA NIPSEY HUSSLE..NI FREEMASONS AU UKIMWI

Image
Los Angeles. Haikuwa wiki nzuri kwa wapenzi wa muziki wa rap duniani baada ya Nipsey Hussle kuuawa katika shambulizi lililofanyika nje ya duka lake la nguo Machi 31, mwaka huu. Hakuwa rapa tu bali mwanaharakati aliyepambana kuhakikisha usawa hasa kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika. Baadhi ya nyimbo zilizomtambulisha ni Blue Laces, Double Up, Crenshaw na Bullets Aint got No Name. Akiwa nje ya duka lake la mavazi Marathon Clothing, alivamiwa na kushambuliwa kwa risasi nyingi na mbili zilimpata kichwani na tumboni na kukatisha safari yake ya miaka 33 hapa duniani. Mshukiwa Erick Holder alikamatwa siku moja baadaye akijaribu kuingia katika hospitali ya wagonjwa wa akili. Mwanamke aliyeendesha gari alilotorokea Holder alijisalimisha polisi akisema hakujua kama mwanaume huyo alilenga kufanya mauaji na alikimbia kuepuka kuuawa na wananchi wenye hasira. Katika mitandao hasa Youtube zimekuwapo taarifa kuwa kifo chake kimetokana na kazi alizokuwa akifanya kwamba baad...